Amesema
Serikali itafanya mapitio ya bodi zote za mazao ya biashara na imeanza
na zao la korosho kisha zao la pamba, tumbaku, kahawa, katani na chai.
Katika tathmini na mapitio hayo , bodi itakayobainika kushindwa
kutekeleza majukumu yake itavunjwa.
Waziri
Mkuu alitoa agizo hilo jana jioni (Jumapili, Oktoba 16, 2016) wakati
akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja
cha Sokoine wilayani Nachingwea mkoani Lindi.
Alisema
anaishangaa bodi hiyo kuacha kutekeleza majukumu yake na kuingilia
minada ya korosho na kuzuia baadhi ya wafanyabiashara wasiweze kununua
zao hilo hali inayoashiria kuwepo kwa watu waliopangwa kununua bila ya
kufuata utaratibu.
“Bodi
leo wamejipa jukumu la kusimamia minada ! sio kazi yao ni kazi ya chama
kikuu, zao la korosho linalimwa kutoka mkoani Ruvuma hadi Tanga,
mtasimamia minada mingapi viachieni vyama vikuu. Vyama vikuu vikiharibu
walalamikaji waje kwenu kama sehemu ya rufaa. Sasa nyinyi mnasimamia
minada mnaharibu walalamikaji watakwenda kwa nani ? kwa nini mng’ang’anie kwenda kwenye minada,” alihoji Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu alisema Ijumaa (Oktoba 14,2016) bodi hiyo ilisitisha
mnada wa korosho Lindi kwa sababu wanunuzi hawakuweka bondi (dhamana ya
mauzo) na alishatoa maagizo ya kuwataka wanunuzi wasiruhusiwe kununua
hadi waweke asilimia 25 ya malipo.
Alisema maagizo hayo aliyatoa tangu mwezi Aprili ila watendaji
wa bodi hiyo hawakuyafanyia kazi kwa wakati na badala yake waliwazuia
wafanyabiashara waliotaka kununua korosho Lindi kwa madai ya kutokuwa na
bondi huku wakiwaruhusu wa Mtwara.
“Kama kule walinunua bila bondi kwa nini wasiwaruhusu na Lindi wakanunua bila bondi ili nijue kwamba mliamua kugoma kuteleza maelekezo ya Serikali? Au hamkumtaka aliyeshinda nyie mlikuwa mnamtaka nani nitashughulika na nyie,” alisisitiza.
Aliongeza
kuwa “Nimesema tukitoa maelekezo lazima yatekelezwe na atakayeshindwa
hatufai, Mheshimiwa mbunge umelalamika juu ya bodi hawa ndio wabeba
maelekezo hatujawahi kuona bodi ya korosho ikienda vijijini kuzungumza
na vyama vikuu hata mara moja,”.
Akizungumzia kuhusu suala la wakulima kulazimishwa kufungua akaunti za
kupitishia malipo yao alisema wasiwalazimishe.“Waelimisheni wakulima
umuhimu wa kufungua akaunti lakini si kwa kuwalazimisha wote wawe na
akaunti hadi yule mwenye kilo tano…na akaunti yenyewe inafunguliwa kwa
sh. 100,000,” alisema.
Alisema
“’wanashindwa kutekeleza niliyowaagiza, halafu wanasingizia utendaji
wao mbovu kuwa ndio maagizo yangu,’ niliwaagiza wapi,” alihoji na
kuongeza kuwa “yapo
makundi yanafanya mambo yanavyotaka alafu yakiwazidi mambo wanasingizia
viongozi wajuu na ndio wale wanaosema kila kitu nimeagizwa kutoka juu,
juu wapi?
“Lazima
tuendelee kudhibiti nidhamu ya vyombo vya tunavyoviunda kwa ajili ya
kuwahudumia wananchi. Tutaendelea kusimamia nidhamu kwa taasisi
zinazowahudumia wakulima nchi nzima,” alisisitiza.
Wakati
huo huo Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi alimkabidhi Waziri
Mkuu msaada wa sh. milioni 16.3 pamoja na nguo kwa ajili ya kusaidia
wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera
Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 17 na
wengine 440 walijeruhiwa.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, OKTOBA 17, 2016
0 comments:
Post a Comment