Jeshi
la kujenga Taifa linapenda kuutaarifi umma juu ya utapeli unaoendelea
kufanywa na baadhi ya watu wanaojifanya wanauwezo wa kuwaingiza vijana
wa kitanzania kwenye mafunzo ya JKT kwa lengo la kuwapatia malipo.
Utapeli huo unafanya kwa njia ya simu za mkononi kwa kutuma ujumbe wa maneno tofauti tofauti.
Jeshi
la kujenga Taifa linasisitiza kuwa ujumbe huo siyo sahihi na wananchi
wanatakiwa kujiepusha na utapeli huo wenye lengo la kujipatia fedha kwa
njia ya udanganyifu.
taarifa za mchakato wa uchukuaji wa vijana wa
kujiunga na mafunzo ya JKT utolewa na makao makuu ya JKT kwa mfumo ulio
rasmi wa Mawasiliano ikiwemo luninga, radio,magazeti na tovuti ya JKT.
Aidha
,JKT kwa kushirikiana na mamlaka ya mawasiliano Tanzania ,inafuatilia
kujua ni mtu gani au kikundi kipi kinahusika na utapeli huo ili hatua
kali za kisheria ziweze kuchukuliwa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment