20 wafa na 65 wajeruhiwa baada ya treni mbili kugongana Pakistan.
Watu 20 wamekufa na 65 wamejeruhiwa baada ya treni mbili kugongana katika Mji wa bandari wa Karachi, Kusini mwa Pakistan.
Taarifa kutoka hospitali zinaeleza kuwa watu zaidi ya 50 wamejeruhiwa katika ajali hiyo na baadhi yao hali zao ni mbaya.
Maafisa waandamizi wa Mji wa Karachi wanasema idadi ya vifo inaweza kuongezeka kutokana na idadi ya abiria waliokuwemo kwenye treni hizo mbili kuwa zaidi ya Elfu-Moja.
Hiyo ni ajali ya pili inayohusisha treni chini ya kipindi cha miezi miwili.
Ajali hiyo imetokea jriani na kituo cha treni cha Landi wakati moja ya treni iliyokuwa ikitokea katika Mji wa Kati wa Multan ilipoigonga kwa nyuma treni nyingine iliyokuwa ikitokea Mji wa Lahore.
0 comments:
Post a Comment