Maelezo ya Naibu spika ni kuwa swali hilo halihusu sera, huku Mbowe akidai linahusu sera kwa kuwa ni rushwa kwa wabunge.
Baada ya Naibu Spika kukataa waziri Mkuu kujibu swali la Mbowe zikaendelea kusikika sauti za chini chini za wabunge, wengine wakisema acha ajibu usimzuie, huku minong'ono ya kila aina ikisikika kuhusu tuhuma hizo.
Kufuatia hatua hiyo katika baadhi ya Maeneo nchini Tanzania, imezuka minong'ono kuwa kwanini Naibu Spika asinge weza kuruhusu waziri mkuu kujibu swali hilo kama maswali mengine huku ikionekana sintofahamu kwamba pengine kuna ukweli juu ya hilo ama la.
Hii ni video ambayo Mbowe aliuliza swali hilo.
0 comments:
Post a Comment