Dar es Salaam.Upande
w Jamhuri kwenye kesi ya Salim Njwete anayetuhumiwa kumwibia Saidi
Mrisho na kumtoboa macho kwa kisu umedai mahakamani hapo kuwa upelelezi
haujakamilika na kuomba siku nyingine ya kukamilisha.
Mshitakiwa Njwete mwenye (34) ambaye ameshitakiwa kwa kumuibia Mrisho na kumjeruhi kwa kumchoma tumboni, mabegani na Machoni.
Taarifa
ya Upelelezi kutokamilika ilielezwa na jana na Mwendesha Mashitaka
Chensensi Gavyole mbele ya hakimu Mkazi Flora Haule kesi hiyo iliyotajwa
na kuangaliwa kama upelelezi umekamilika.
"Mshitakiwa yupo
mbele ya Mahakama hii lakini upelelezi bado haujakamilika, tunaomba
Mahakama itupangie siku nyingine ya kutajwa kutokana na upelelezi
kuendelea" alisema Gavyole.
Kutokana na sababu hizo, Hakimu Haule aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 16 itakapo tajwa tena.
Mshitakiwa
huyo maarufu kama Scopioni alifikishwa Mahakamani hapo akiwa kwenye
gari dogo la mizigo tofauti na siku za nyuma ambapo alikuwa akiletwa
akiwa kwenye basi la Magereza.
Awali alidaiwa kuwa mshitakiwa
alitenda kosa hilo Septemba 9 Buguruni Sheli alipomuibia Mrisho fedha na
vitu vyenye thamani ya Sh.476,000 na kumjeruhi kwa kumchoma kisu
tumboni, mabegani na machoni.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment