Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma
Serikali
kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
imejipanga kufungua ofisi ya ubalozi mdogo katika mji wa Guangzhou
uliyopo nchini China ili kongeza fursa za kibiashara pamoja na
kurahisisha huduma mbalimbali Watanzania wanaoishi nchini humo.
Hayo
yamesemwa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Suzan
Kolimba alipokuwa akijibu swali la Mhe. Machano Said aliyehoji juu ya
kuwekwa kwa ubalozi wa Tanzania nchini China pamoja na utaratibu
unaotumika katika kuwapa Visa wananchi ambao wameaamua kuishi nchini
humo.
Mhe. Dkt Kolimba amesema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya
Serikali ya China kuchagua majimbo matatu ya Jiangsu, Zhejiang pamoja na
Guangdong ili yawe na uhusiano maalum na nchi tatu za Afrika ambapo
Tanzania ni moja ya nchi hizo.
“Tunaamini kuwa kwa kufungua ofisi
za ubalozi katika mji huu Tanzania itakuwa na fursa ya kuyashawishi
makampuni ya mji huo kuja kuwekeza katika nchi yetu pamoja na kutoa
huduma mbalimbali kwa Watanzania wanaofanya biashara katika mji huo”,
alisema Dkt. Kolimba.
Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa mahusiano
ya kimataifa ni njia mojawapo ya kuimarisha shughuli za kibiashara na
kijamii miongoni mwa wananchi wa nchi hizo mbili katika kuwaletea
maendeleo.
Akiongelea kuhusu Watanzania walioamua kuishi nchini
china, Dkt Kolimba amebainisha kuwa utaratibu uliopo sasa kwa wananchi
wanaoishi zaidi ya mwaka mmoja katika nchi hiyo wanatakiwa kuwa na
kibali cha kuishi nchini humo.
Aidha, Dkt. Kolimba amefafanua kuwa
kibali hicho kinapatikana kwa kuwasilisha maombi kwenye wizara
inayoshughulika na masuala ya mambo ya ndani ya China na iwapo watakuwa
wamekidhi vigezo vinavyotakiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi
hiyo watapatiwa vibali hivyo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment