WAZIRI wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Salama Aboud Talib, amesema Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), limefuata taratibu zote hadi kufikia uamuzi wa kutangaza ongezeko la bei ya umeme kwa wateja wake.
Talib ametoa ufafanuzi huo baada ya baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kupinga ongezeko la umeme lililotangazwa na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) hivi karibuni.
Mwakilishi wa Jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub aliwasilisha hoja binafsi mbele ya Baraza la Wawakilishi akiitaka serikali kusitisha mpango wa kuongeza bei ya umeme kwa wananchi kwani kufanya hivyo ni sawa na kuwabebesha mzigo mkubwa wananchi huku zikiwapo taasisi na Wizara za Serikali zikidaiwa malimbikizo makubwa ya madeni.
Akifafanua Talib alisema, Zeco iliomba kuongeza bei ya umeme kwa zaidi ya miaka miwili nyuma, lakini ilikataliwa kufanya hivyo kutokana na sababu za kiuchumi.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilshi, wameitaka serikali kuzibana wizara zake ili zilipe malimbikizo ya madeni yanayofikia Sh bilioni 21, ambayo shirika hilo la umeme inazidai taasisi mbalimbali za serikali na wizara.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment