Image
Image

Jeshi la Nigeria laendesha operesheni na kuwaokoa mateka 85 kutoka mikononi mwa Boko Haram

Watu 85 wanaojumuisha watoto na wanawake wameokolewa kutoka mikononi mwa kundi la Boko Haram kwenye operesheni iliyoendeshwa na jeshi la Nigeria katika mkoa wa Rorno ulioko maeneo ya karibu na ziwa Chad.Wanamgambo 5 wa Boko Haram pia wameripotiwa kuangamizwa na jeshi kwenye operesheni hiyo katika eneo la Chukungudu kaskazini mwa nchi.
Kulingana na maelezo yaliyotolewa na jeshi la Nigeria, operesheni hiyo iliarifiwa kuendeshwa kwa mafanikio katika maeneo ya Geram, Bulankassa na Chukungudu ambapo kambi za wanamgambo ziliharibiwa.
Maelezo zaidi yanaarifu kwamba mateka hao waliweza kuokolewa pamoja na jengo moja lililokuwa likitumiwa kutengezea mabomu na vilipuzi.
Tangu mwaka 2000 ambapo kundi la Boko Haram lilianza kuendesha harakati za kigaidi na kutekeleza mashambulizi kufuatia kifo cha kiongozi wake Muhammed Yusuf mwaka 2009. Watu zaidi ya elfu 17 wameripotiwa kupoteza maisha kufuatia mashambulizi ya Boko Haram huku wengine wengi wakiwemo wanajeshi wakitekwa nyara.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment