Kwa mujibu utafiti uliofanyika umedhihirisha kuwa kwanzia mwaka 2030
kila mwaka wanawake takriban milioni 5.5 watafariki kila mwaka kutokana
na maradhi ya saratani.Ripoti ya utafiti kuhusu ugonjwa huo
iliwasilishwa na shirika la American Cancer Society katika Kongamano la
mwaka huu kuhusu maradhi ya saratani liliondaliwa jijini Paris nchini
Ufaransa lilibainisha kuwa waathirika wengi wa maradhi haya wapo katika
nchi zenye mapato ya chini na nyuma kiuchumi.
Katika ripoti hiyo
imeonyesha pia kuwa na ongezeko la vifo,ongezeko la idadi ya
wazee,matatizo ya unene na pia ukosefu wa lishe bora .
Vile vile ripoti hiyo imebainisha kuwa wanawake wanaathiriwa zaidi na ugonjwa wa saratani.
Kulingana
na utafiti ulioonyeshwa katika ripoti hiyo mnamo mwaka 2012 watu
milioni 8 walifariki kutokana na saratani na kati yao milioni 3.5
walikuwa wanawake .
Wanawake 1.7 wamefariki kutokana na saratani ya matiti .
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment