Hata hivyo Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kufuatia kifo
cha Spika Mstaafu na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Urambo lililopo Mkoani Tabora
Mhe. Samwel Sitta.
Mhe. Samwel Sitta
amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Technical University
of Munich nchini Ujerumani alikokuwa akipatiwa matibabu tangu mwezi uliopita.
Katika salamu
hizo, Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa
za kifo cha Mhe. Samwel Sitta na kwamba Taifa limempoteza mtu muhimu aliyetoa
mchango mkubwa katika uongozi na maendeleo.
“Nitamkumbuka Mzee
Sitta kwa uchapakazi wake, uzalendo wake na tabia yake ya kusimamia ukweli
katika kipindi chote alichokuwa kiongozi katika ngazi mbalimbali za siasa na
Serikali.
“Kupitia kwako
Mhe. Spika naomba kutoa pole nyingi kwa Mke wa Marehemu Mhe. Magreth Sitta
ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Urambo na familia nzima ya marehemu, Wabunge wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wananchi wa Urambo Mkoani Tabora na
watu wote walioguswa na msiba huu” amesema Rais
Magufuli katika salamu hizo.
Dkt. Magufuli
amesema anaungana na wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo na
amewaombea moyo wa uvumilivu na ustahimilivu.
“Namuomba Mwenyezi
Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi, Ameni”
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es
Salaam
07 Novemba,
2016
0 comments:
Post a Comment