BALOZI wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem, amesema nchi yake imeandaa
ziara ya kiserikali kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Dk Augustine Mahiga, kuitembelea nchi hiyo ili
kukamilisha mikataba ya ushirikiano kati ya nchi hiyo na Tanzania.
Balozi Al Najeem alisema hayo kwenye hafla aliyoiandaa kwa ajili ya
kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutimiza mwaka mmoja. Hafla
hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na
mabalozi wa nchi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania.
Alisema tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani imeimarisha
ushirikiano na Kuwait kwa kuanzisha ubalozi wa nchini humo na kuwepo
kwa balozi kumerahisisha na kuhamasisha wawekezaji wa Kuwait kuja
kuwekeza Tanzania na wafanyabiashara kuleta bidhaa zao na kuagiza bidhaa
za kilimo kupata soko nchini Kuwait.
Mikataba inayokusudiwa kusainiwa wakati wa ziara ya Waziri Mahiga
nchini humo, itahusu ushirikiano katika nyanja ya uchumi ikiwemo wa
kutotoza kodi mara mbili kwa bidhaa zinazoingia katika nchi hizi mbili,
kukuza kiwango cha biashara na kusaidia sekta huduma za kijamii.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Balozi Mahiga ameipongeza Kuwait kwa
misaada ya kibinadamu na ya kiuchumi kwa Tanzania na kusisitiza kuwa
Kuwait inastahili heshima ya kuwa kituo cha misaada ya kiutu duniani.
Aidha, aliishukuru kwa kuitikia haraka mwito wa kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, Septemba mwaka huu.
Home
News
Slider
Ziara ya kiserikali kukamilisha mikataba ya ushirikiano kati ya Kuwait na Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment