Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais, inawataarifu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli ametia saini Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
iliyopitishwa na Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano
wake wa 5 Mjini Dodoma.
Rais Magufuli
amesaini Sheria hiyo tarehe 16 Novemba, 2016.
Dkt. Magufuli
amewapongeza wadau wote kwa kufanikisha kutungwa kwa Sheria hiyo.
"Naamini kuwa
Sheria hii itasaidia kuboresha sekta ya habari kwa manufaa ya wanataaluma
wenyewe na Taifa" amesema Rais Magufuli.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es
Salaam
17 Novemba,
2016
0 comments:
Post a Comment