HATIMAYE rufaa ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema iliyokatwa na mawakili wake itasikilizwa Jumatatu ijayo.
Rufaa
hiyo itasikilizwa na Jaji Fatma Masengi ya kuomba mbunge huyo kupewa
dhamana baada ya mawakili wanaomtetea jana kusajili maombi ya rufaa
namba 112/113 ya mwaka 2016 Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, ili kudai haki
ya dhamana ya Lema aliyonyimwa kutokana na makosa ya kisheria
yaliyofanywa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.
Rufaa hiyo imepokewa
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha na kupangwa kwa Jaji Masengi ambaye ndiye
atakayeamua hatma ya Lema kuwa nje kwa dhamana au la.
Akizungumza na
gazeti hili, mawakili hao ambao ni Sheck Mfinanga na Peter Kibatala
walisema tayari wamesajili rufaa yao Mahakama Kuu na wanasubiri siku
hiyo ili isikilizwe.
Mfinanga alisema wameamua kufungua maombi ya
rufaa kwa ajili ya kujua ni kwa nini Lema amekosa dhamana ambayo awali
Hakimu Desdery Kamugisha alisema ipo wazi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment