WAISLAMU wote nchini wametakiwa kuadhimisha Siku ya Maulid kwa kufanya usafi, kupanda miti na kuchangia damu.
Aidha, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Siku ya Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W).
Hata hivyo, ugeni rasmi wa Waziri Mkuu Majaliwa unategemea ratiba yake.
Hayo
yalisemwa jana Dar es Salaam na Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakar
Zubeir wakati akizungumzia Siku ya Maulid ambayo alisema kwa mwaka huu,
Maulid itasomwa usiku wa Desemba 11, na kitaifa itafanyika Kata ya
Shelui wilayani Iramba Mkoa wa Singida na mapumziko yatakuwa siku
inayofuata yaani Desemba 12.
Mufti Zubeir alisema Waislamu wanatakiwa
kutumia siku hiyo kuonesha matendo mema na yenye kumpendeza Mwenyezi
Mungu pamoja na kuisaidia jamii kufanya usafi kwenye mitaa yao na
kuchangia damu ili kusaidia wenye uhitaji huo.
Alisema anatakiwa
kiongozi kufanya matendo hayo wanapoifurahia siku ya kuzaliwa Mtume
Muhammad (S.A.W) ambaye amesema uislamu ni usafi, basi jisafisheni
wenyewe.
“Mimi na familia yangu tutafurahia siku hiyo kwa kufanya
usafi mtaani kwetu Mikocheni na kuchangia utoaji damu ili kusaidia watu
wenye uhitaji,” alieleza Mufti Zubeir na kuwataka Waislamu
kutokujiingiza kwenye makundi ya ugaidi kwani Uislamu sio ugaidi na
kuwasihi waachane na hizo tabia.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment