Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa
muda wa mwezi Mwezi Moja kuanzia leo tarehe 18-Nov-2016 kwa watendaji na
viongozi waandamizi wa wilaya ya Ilemela wahamie kwenye wilaya hiyo
haraka iwezekanavyo na waache tabia ya kukaa kwenye wilaya nyingine kwa
kisingizio cha kukosa nyumba za serikali.
Makamu wa Rais ametoa agizo
hilo katika hotuba yake kwa wananachi na watendaji wa Halmashauri ya
Manispaa ya Ilemela waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi jengo la
utawala la Manispaa hiyo na kukabidhi madawati 1,074 yaliyotolewa na
ofisi ya Bunge.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha kukerwa
na tabia hiyo na amewataka viongozi hao wahamie karibu na maeneo yao ya
kazi kabla ya muda aliotoa kwisha ili waweze kuwa karibu na wananchi
katika kuwasaidia kutatua kero na matatizo yanayowakabili kwa haraka.
Akiwa
katika wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza wakati anaweka jiwe la msingi
katika mradi wa ukarabati wa mchinjio ya Nyakato jijini Mwanza, Makamu
wa Rais ameuagiza uongozi jiji la Mwanza kusimamia kikamilifu mradi wa
ukarabati wa machinjio ya Nyakato na watendaji watakaobainika kuhujumu
mradi ambao utagharimu zaidi ya shilingi bilioni Tatu wachukuliwe hatua
kali za kisheria.
Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo katika hotuba yake
kwa wananchi na watendaji wa jiji la Mwanza waliohudhuria hafla ya
uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa ukarabati wa machinjio ya Nyakato
unaohusisha uboreshaji wa jengo la machinjio,tanki la kuhifadhi
maji,ujenzi wa vyumba vya baridi vya kuhifadhi nyama na ujenzi wa mtambo
wa kutibu majitaka yanayotoka kwenye machinjio hiyo.
Makamu wa Rais
katika hotuba yake, amesema hategemei hata kidogo ukarabati wa machinjio
hiyo ufanyike chini ya kiwango kwa sababu ni mradi wa kibiashara ambao
ukikamilika na kuanza kufanya kazi utasaidia jiji la Mwanza kupata
mapato yatakayosaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi.
Makamu
wa Rais pia amemwagiza Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ahakikishe
anasimamia uundaji wa menejimenti ya machinjio hiyo ambayo itafanya kazi
vizuri na sio kuingiza watu ambao hawana uwezo ambao watakwamisha
utendaji kazi wa machinjio hiyo.
Kuhusu ukusanyaji wa kodi, Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan amewahimiza watendaji wa Halmashauri zote za
mkoa wa Mwanza waongeze kasi ya ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa
njia ya kielekroniki kutoka kwenye vyanzo mbalimbali fedha ambazo
zitasaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi mkoani humo.
Makamu
wa Rais pia ametoa wito maalum kwa wananchi nchini wahakikishe wanadai
risiti wanaponunua bidhaa mbalimbali kwani kufanya hiyo watasaidia
kuongeza mapato yake ambao yataelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.
Katika
Mkutano wake wa Majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya Siku Tano mkoani
Mwanza na viongozi wa mkoa wa Mwanza, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
amewasisitiza viongozi na watendaji wa mkoa wa Mwanza wafanye kazi kwa
bidii katika kuwatumikia wananchi kwa kuzingatia kanuni na taratibu za
umma.
Ameonya kuwa serikali ya awamu ya Tano haitasika kuwachukulia
hatua kali viongozi na watendaji ambao watakwenda kinyume na maadili ya
utumishi wa umma kwenye maeneo yao ya kazi.
Makamu wa Rais Samia
Suluhu Hassan amewataka viongozi wa mkoa wa Mwanza kusimamia kikamilifu
katika kulinda hali ya amani na Utulivu na wachukue hatua kali kwa watu
wanaotaka kuharibu amani ya nchi.
Makamu wa Rais amehitimisha ziara
yake ya kikazi ya siku Tano mkoani Mwanza kwa kukagua,kuzindua na
kuweka mawe ya msingi katika miradi ya mbalimbali ya maendeleo katika
wilaya za Ilemela,Misungwi, Kwimba, Magu na Nyamagana.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Mwanza.
18-Nov-2016.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment