WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema
Serikali ya Awamu ya Tano itahakikisha mashindano ya ulimbwende yanakuwa
na thamani na yenye faida.
Nape aliyasema hayo wakati akimkabidhi bendera ya Taifa, Miss Ilala
2016, Julitha Kabete ambaye pia ni mshiriki wa mashindano ya Miss
Tanzania 2016, ambaye anakwenda kushiriki mashindano ya urembo Afrika
yatakayofanyika Novemba 26 katika kitongoji cha Calabar nchini Nigeria.
“Tunataka mashindano ya Miss Tanzania ambaye anafaidika sio mshindi
peke yake tumeona hapa huyu alikuwa mshindi wa nne na amepata nafasi ya
kuwakilisha nchi, tunafahamu mashindano ya Miss Tanzania yalikuwa
yamefungiwa kufanyika ila sasa yamerudi vizuri, tutaendelea kuyaimarisha
yawe bora na matarajio ya serikali ni kuona tunakuwa tunafanya vizuri
na siku moja hata mshindi wa Miss World atoke Tanzania,” alisema Nape.
Pia Nape alisema serikali inamtakia safari njema na ipo nyuma yake kumpa msaada pindi unapohitajika.
Akizungumza wakati wa kukabidhiwa Miss Julitha Kabete amesema
amejiandaa kwa ajili ya mashindano hayo na anaamini atafanya vizuri
kwenye mashindano hayo ambayo ndio kwanza yanaanza.
“Naomba Watanzania wanisapoti ili nifanikiwe kushinda Miss Africa
ambayo inafanyika Nigeria, ni nafasi ya kipekee ambayo nimepata na
nikipata ushindi ni wetu sote,” alisema Julitha.
Mashindano hayo yatafanyika kwa mara ya kwanza Afrika katika
kitongoji cha Calabar kilichopo Nigeria. Naye mrembo huyo akizungumza
katika hafla hiyo alisema kuwa amejiandaa vizuri kwa ajili ya shindano
hilo la kwanza kufanyika.
Home
MICHEZO
Slider
Serikali:Tutahakikisha mashindano ya ulimbwende yanakuwa na thamani na yenye faida.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment