TIMU ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ imewaduwaza Wacameroon juzi
baada ya kuifunga timu yao kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kimataifa wa
kirafiki uliochezwa juzi usiku kwenye Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Omnispo
mjini Younde.
Huo ulikuwa mchezo wa pili uliochezwa baada ya ule wa kwanza
uliochezwa siku mbili kabla, ambapo Twiga Stars walifungwa mabao 2-0.
Katika mchezo huo ulioshuhudiwa na umati mkubwa wa mashabiki wa
Cameroon, wenyeji ilitangulia kufunga bao la kuongoza lililowekwa
kimiani na Agnes Nkada kabla ya Mwanahamisi Omary kusawazisha na baadaye
kufunga la ushindi.
Mchezo huo ulikuwa na lengo la kukipima kikosi hicho cha Cameroon
kinachojiandaa na michuano ya fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) kwa
wanawake zitakazofanyika kuanzia Novemba 19 hadi Desemba 3, mwaka huu.
Tayari Cameroon iliwahi kucheza pia na Kenya na kushinda bao 1-0 kama
sehemu ya maandalizi hayo. Cameroon inatarajiwa kuchuana na Misri
katika mchezo wa ufunguzi utakaochezwa Novemba 19, kwenye uwanja huo
uliopo mjini Younde, wakati Afrika Kusini iliyopo Kundi B itachuana na
Zimbabwe siku hiyo.
Timu hiyo ya Cameroon ipo Kundi A pamoja na Afrika Kusini, Zimbabwe
na Misri wakati Kundi B lina timu za Nigeria, Ghana, Mali na Kenya.
Twiga Stars chini ya Kocha Sebastian Nkomwa imeendelea kujiwekea
rekodi bora, kwani ndio mabingwa wa Kombe la Afrika Mashariki na Kati,
Kombe la Chalenji.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment