Amesema makubaliano yanaweza kuhitaji mazungumzo ya siku zaidi ya moja
Rais huyo wa Liberia ambaye ameongoza ujumbe wa Marais wenzake wa ukanda wa Afrika Magharibi na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa amesema wamekwenda Banjul kuwasaidia wananchi wa Gambia kupata ufumbuzi wa mgogoro unaoikabili nchi yao.
Amesema suala hilo limekuwa gumu baada ya Rais JAMMEH kuwasilisha suala la matokeo ya uchaguzi wa Rais kwenye Mahakama Kuu kutaka kubatilisha matokeo yaliyompa ushindi kiongozi wa upinzani,ADAMA BARROW.
Wakati huo huo, Chama kinachotawala nchini Gambia kimesisitiza kurudiwa kwa uchaguzi wa Rais nchini humo hapo jana wakati viongozi wa Umoja wa Uchumi wa Afrika Mgharibi na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa wakiwasili nchini humo kumshawishi Rais YAHAYA JEMMEH kukabidhi madaraka kwa Rais mteule, ADAMA BARROW.
0 comments:
Post a Comment