WANASAYANSI duniani wamesema kujifungua mtoto kwa njia ya upasuaji kunaimarisha maumbile.
Wanawake wengi wanajifungua watoto kwa njia ya upasuaji kwa sababu njia ya kizazi kuwa nyembamba.
Watafiti
walikadiria kuwa visa ambavyon mtoto anashindwa kupita katika njia ya
uzazi vimeongezeka kutoka 30 kwa kila vizazi 1,000 katika miaka ya 1960
hadi visa 36 kwa kila vizazi 1,000 leo hii.
Kabla ya njia hii ya upasuaji kuanza kutumika, wanawake wengi walikuwa wakifariki dunia wakati wa kujifungua.
Lakini
pia wanasayansi kutoka Austria walioendesha utafiti huu, walisema vifo
vya wanawake wakati wa kujifungua vimepunguzwa kwa sababu ya upasuaji.
Hata hivyo, imegunduliwa kwamba mwanamke aliye na njia nyembamba ya kizazi huenda pia mwanawe wa kike akarithi hali hiyo.
Watafiti walisema visa vya watoto kushindwa kuzaliwa kwa njia ya kawaida vimeongezeka kwa kati ya asilimia 10 na 20.
Utafiti huo umechapishwa na jarida Taasisi ya Taifa ya Sayansi (NAM) ya Marekani.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment