Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, linakutana jijini Kinshasa kutathmini hatua iliyopigwa kuhakikisha mkataba wa kisiasa uliokubaliwa mwezi Desemba mwaka 2016, unaanza kutekelezwa kikamilifu.
Mkutano huu unafanyika wakati huu kukiwa na mvutano kati ya wanasiasa wa upinzani na serikali kuhusu namna ya kugawana madaraka.
Nao muungano wa vyama vinavyomuunga mkono rais Joseph Kabila, umezindua mpango maalum unaonekana kama hatua ya kwanza kuelekea uteuzi wa mtu atakayemrithi rais Joseph Kabila, baada ya muda wake kumalizika kufikia mwisho wa mwaka huu.
Katika hatua nyingine, Msemaji wa wanasiasa wa upinzani wa G7 Christophe Lutundula amesema wameendelea kutoa wito kwa Muungano wa wanasiasa wanaopinga mkataba huo wa kisiasa kuukubali.
Umoja wa Mataifa pia umewataka wadau wa kisiasa nchini humo kuheshimu makubaliano hayo ili mwafaka upatikane katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati.
Upinzani unaoongozwa na Ettiene Tshisekedi, kwa mujibu wa mkataba huo, unatoa nafasi ya Waziri Mkuu ambayo kwa sasa anashikiliwa na Samy Badibanga, ambaye ameonekana kupinga mkataba huo.
Home
Kimataifa
Slider
Baraza la Maaskofu DRC kukutana Kinshasa kujadili kutekelezwa mkataba wa kisiasa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment