Image
Image

Serikali nchini Kenya yawashukia Madaktari waliogoma, yawapa muda la sivyo inawafuta kazi.

SERIKALI nchini Kenya imewataka Madaktari wanaogoma kurudi kazini kufikia siku ya Jumatano wiki hii la sivyo wafutwe kazi.
Hatua ambayo inakuja baada ya Madaktari hao ambao wamekuwa wakigoma tangu mapema mwezi Desemba mwaka 2016, kukataa pendekezo la serikali kuwaongezea mshahara kwa asilimia 40.
Mwenyekiti wa Baraza la Magavana nchini humo Peter Munya, amezitaka serikali za Kaunti nchini humo kuwa tayari kuanza zoezi la kuwaajiri Madaktari wapya ikiwa wanaogoma hawatarudi kazini.
Wiki iliyopita, rais Uhuru Kenyatta alikutana na wawakilishi wa Madaktari hao katika Ikulu ya Mombasa na kuwaomba kukubali nyongeza ya mshahara ya asilimia 40, pendekezo ambalo lilikataliwa na wahudumu hao wa afya.
Waziri wa afya Cleopa Mailu amesema licha ya kuzungumza na viongozi wa Madaktari hao, kuwasihi ili kuwahimiza  zaidi ya Madktari 3,000 wanaogoma kurudi kazini ili kuwapa huduma wagonjwa wanaoteseka, juhudi zao hazijafanikiwa.
Mahakama Kuu jijini Nairobi siku ya Jumanne, iliamuru kukamatwa kwa wawakilishi wa Madaktari hao baada ya kutofika Mahakamani kusikiliza kesi inayowakabili.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment