Akizungumza kwa njia ya simu Dalali Abdala ambaye ni mvuvi amesema nikweli walishuhudia tukio hilo nakusema kuwa wakati wakiwa baharini hapo waliona
miili ya watu iki elea ndipo wakasogea karibu na kuona Mashua iliyokuwa imebeba watu imezama,ndipo wakafanya juhudi za kuokoa watu waliokuwa hai ambao walikuwa wakiomba msaada na baadae ndio walipo maliza kuokoa wakiokuwa hai na ndipo wakaanza wale waliofariki.
"Hii sio Boti, Nikweli kwamba Mashua ilikuwa imebeba abiria imezama na huenda tu ni hali ya hewa yaani upepo umegeuka na sisi tupo baharini huku ndipo tulivyoona hivyo ikabidi tusaidie kuokoa waliopo hai ndipo turudi kuwatoa waliokufa na tukafanikiwa, ndio muda si mwingi police marine ikaja ikasaidiana nasi ikaokoa"Amesema Dalali Abdala.Dalali abdala amesema kuwa shughuli ya kuanza kuokoa iliwabidi mara baada yakuona hali sio shwari, ndipo baada ya muda Police Marine nao walifika ili kuendelea na uokozi ambapo ajali hiyo ilitokea afajiri mwendo wa saa kumi na moja unusu leo.
Hata hivyo mvuvi huyo Dalali Abdala amesema kuwa mara baada ya shughuli ya uokozi kumalizika basi Boti ya Police Marine ilichukua miili na kuipeleka katika hospitali ya Bombo mkoani Tanga.
Tunamtafuta Kamanda wa Polisi Tanga kwa taarifa zenye uthibitisho zaidi.
0 comments:
Post a Comment