Image
Image

Ditto afunguka sababu za kuimba Moyo Sukuma Damu, awanyooshea kidole wasanii wenye lugha chafu.

Dar es Salam.
Msanii wa Bongo Flava nchini Lameck Ditto anayetamba na wimbo wake wa Moyo Sukuma Damu, leo 18 January 2017 amesema kuwa Tageti yake kimuziki kwanza nikuhakikisha kwamba muziki wake unafahamika kwanza nyumbani ndipo avuke ng'ambo,huku akisema kuwa Video yake ya moyo sukuma damu ameifanya hapa hapa nyumbani kutokana na Director Travellar wa Kwetu Studio kuwa mwenye kufanya Video Nzuri.
Akizungumza kupitia Radio One Stereo Ditto ameweka wazi swali ambalo limekuwa likiwatatiza wengi juu ya sababu za kuimba Moyo Sukuma damu kwamba huenda inalandana na Maisha yake lakini amevunja ukimya kwa kusema kuwa huwa anaimba kitu ambacho kinawazunguka wengi katika jamii na ndio maana kila anayeusikia wimbo huo humgusa.
Changamoto katika muziki amesema zipo lakini haziwezi kukwepeka na kuwepo ndio kunakofanya kwamba aendelee kukazana kuimba wimbo mzuri na wenye maudhui yanayo mgusa kila mmoja hivyo changamoto ni chachu ya mafanikio.
Ditto ameongeza kuwa wikimbili zijazo ataanza kushuti wimbo wake mpya, licha ya kuwa hakuutaja ni wimbo gani nakuwataka mashabiki kuendelea kumuunga mkono,kuhusu kuoa na kushuka kimuziki amesema kuwa inategemea na wanafamilia wenyewe namna wanavyojipanga tu.
Aidha Amewataka wasanii wenzake kufanya muziki huo kwa heshima na busara bila matusi kupitia kurasa mbalimbali za kijamii, bali tu watambue kuwa muziki huo ni biashara ili iwe alama kwa wasanii wachanga ambao wanajifunza kutoka kwao huku wakitamani kufika walipo, hivyo wakifanya mambo yasiyo mema watakuwa hawawafundishi kitu wasanii wachanga.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment