kutoka mkoani humo.
Piaameziagiza halmashauri nchini kushirikiana na Idara ya Ukaguzi
ili kuhakikisha
wanawasimamia vizuri walimu jambo litakalowezesha kuboresha
ufundishaji na hatimaye kupata
matokeo mazuri.
WaziriMkuu ametoa agizo hilo Januari 17, 2017 wakati akizungumza
na watumishi na wananchi wa mkoa wa Katavi alipowasili Ikulu ndogo ya Mpanda kwa ajili ya
kufungua duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda.
Kwamujibu wa matokeo hayo kati ya
shule 10 za sekondari zilizofanya vibaya
kwenye mtihani huo, tisa zinatoka katika Mkoa wa Mtwara na moja
Tanga.
Shule za Mtwara zilizofanya vibaya ni Chingungwe, Malocho,
Naputa, Chanikanguo,
Mtiniko, Michiga, Msimbati, Salama na Lukodoka huku ya
Tanga ikiwa ni Nywelo.
“Viongozi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia pamoja na Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) waende Mtwara,wakafuatilie
kwakina wajue kuna nini hadi shule tisa kati ya 10 zilizofanya
vibaya katika matokeo ya mitihani ya kidato cha pili mwaka jana zitoke
huko,” amesisitiza.
Mbali na kuuagiza huongozi wa wizara hizo kwenda mkoani Mtwara pia
Waziri Mkuu
amewataka wasimamie vizuri mikoa ambayo awali ilikuwa na matokeo mabaya na sasa inafanya vizuri na
wahakikishe shule za mikoa hiyo
hazishuki na badala yake ziendelee
kupata matokeo mazuri zaidi.
Awali,akisoma taarifa ya mkoa huo, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja
Jenerali
Mstaafu, Raphael Muhuga alisema katika matokeo ya mtihani kidato
cha
pili ya mwaka jana mkoa wake ulishika nafasi ya pili kitaifa
ukiongozwa
na mkoa wa Geita.
Alisema kwa sasa wanajipanga kuhakikisha katika mitihani ya mwaka
huu wanashika nafasi ya kwanza kitaifa, hivyo alitoa wito kwa watendaji wa
Idara ya Elimu, wakuu wa shule, wazazi na walezi kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha malengo hayo
yanafanikiwa.
0 comments:
Post a Comment