Image
Image

GAMBIA:Jammeh saa zake zinahesabika za kung'olewa kinguvu na Jeshi.

Viongozi wa nchi za Afrika Magharibi wamempa Yahya Jammeh fursa ya mwisho kuachia madaraka, huku wanajeshi wa Senegal wakiingia nchini Gambia.
Bw Jammeh amepewa hadi saa sita mchana Ijumaa ya leo 20 January 2017  anatakiwa kuachia madaraka la sivyo aondolewe kwa nguvu na wanajeshi wa nchi za Afrika Magharibi wanaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
Wanajeshi hao wametakiwa kusubiri hadi muda aliopewa umalizike ndipo waanze kutumia nguvu ya kumuondoa.
Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (Ecowas) inaunga mkono Adama Barrow, ambaye aliapishwa kuwa rais mpya wa Gambia katika ubalozi wa nchini hiyo nchini Senegal.
       Jammeh aongezewa jina jingine
Juhudi za mwisho za kumshawishi Bw Jammeh kuondoka kwa hiari, ambazo zinaongozwa na Rais wa Guinea Alpha Conde, zinatarajiwa kufanyika Ijumaa asubuhi.
Mwenyekiti wa tume ya Ecowas, Marcel Alain de Souza, alisema iwapo mkutano huo utakaoongozwa na Bw Conde hautafaulu, basi hatua ya kijeshi itafuata.
"Iwapo kufikia saa sita mchana, yeye (Bw Jammeh) hatakubali kuondoka Gambia chini ya Rais Conde, tutaingilia kijeshi," amesema.
Habari za kuapishwa kwa Adama Barrow zilipokelewa kwa furaha na shangwe Banjul.
Adama Barrow baada ya kuapishwa aliwaamuru wanajeshi wa Gambia wasalie kambini.
Adama Barrow, mtu aliyeibuka mshindi katika uchaguzi wa urais nchini Gambia ameapishwa rasmi kuwa rais wa taifa hilo.
Alikula kiapo hicho katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal 19 January 2017 huku akiwaagiza wanajeshi wa Gambia kusalia katika kambi zao.
Ametambuliwa kimataifa.
Lakini aliyekuwa rais wa taifa hilo Yahya Jammeh amekataa kujizulu na muda wake wa kuhudumu umeongezwa na bunge.
Viongozi wa Afrika Magharibi wameshindwa kumsihi bw Jammeh kuondoka mamlakani.
Wametishia kumuondoa kwa nguvu.
Bw Jammeh alishindwa katika uchaguzi huo wa Disemba mosi ,kulingana na tume ya uchaguzi nchini humo.
 Lakini anataka matokeo ya uchaguzi huo kufutiliwa mbali akidai makosa mengi katika uchaguzi huo.
 ''Mimi Adama Barrow ,naapa kwamba nitatekeleza wajibu wangu katika afisi ya urais wa taifa la Gambia kwamba nitahifadhi na kutetea katiba'' .
Na katika hotuba yake ya kuapishwa ,aliwaagiza wanachama wote wa jeshi la gambia kusalia katika kambi zao. ''Wale watakaopatikana wakibeba silaha watachukuliwa kuwa waasi'', alionya.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment