Maelfu ya watu wameadamana katika miji ya New York na Washington nchini Marekani kumpinga Donald Trump ambaye leo anaapishwa kuwa rais wa Marekani.
Katika mkesha wa kuapishwa Trump, maelfu ya watu wenye hasira wameandamana New York mbale ya jengo linalomilikwa na bilionea huyo wakilaani sera zake zenye utata na wakiapa kuvuruga sherehe za kuapishwa kwake.
Inatazamiwa kuwa watu karibu milioni moja, wakiwemo waungaji mkono na wapinzani wa Trump, watajitokeza mitaani Washington wakati wa kuapishwa kwake kama rais mpya wa Marekani. Kuna wasi wasi kuwa makundi hayo mawili yanaweza kupigana na kusababisha maafa.
Trump amewachukiza Wamarekani wengi kutokana na matamshi yake ya kuwatusi na kuwakejeli wanawake, wahamiaji hasa wenye asili ya Afrika na Asia, Waislamu na makundi mengine ya walio wachache Marekani.
Pamoja na kuwa Trump ametoa mwito wa umoja wa kitaifa kabla ya kuapishwa kwake, tayari wabunge 40 wa chama cha upinzani cha Democrat wametangaza nia yao ya kususia sherehe za kuapishwa Trump.
Home
Kimataifa
Slider
Maelfu wa watu waandamana kupinga kuapishwa kwa TRUMP New York na Washington Marekani.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment