Katika kuhakikisha kuwa elimu inakuwa bora, jamii za wakulima na wafugaji walioko katika vijiji vya Msua,Kwala na Mpera Mumbi Kibaha vijijini wananchi mbali mbali wameshauliwa kujitokeza kusaidia watoto wasiojiweza na wazazi wao katika vijiji hivyo kwa kukosa kipato cha kuwanunulia vifaa vya shule kama madaftali.
Kauli hiyo imekuja muda mchache mara baada ya kupatiwa vifaa mbalimbali vya shule yakiwamo Madaftari na nguo za Shule wazazi wa watoto 100 kutoka kwa wadau mbali mbali wa elimu kwa kushirikiana na serikali za vijiji hivyo.
Wadau hao ambao ni Daniel Simba na Loyce Nducha amabao ni wachungaji katika kanisa la kilutheri Tanzania Wamesema kuwa hari ya elimu inaendelea kuimarika kutokana na Serikali kufuta michango mashuleni iliyokuwa inasababisha wazazi wengi kukosa na kusababisha watoto wengi kutokwenda shule.
0 comments:
Post a Comment