Image
Image

KAYA 704 mkoani Arusha zaondolewa kwenye mpango wa TASAF kwa kukosa sifa.

KAYA 704 mkoani Arusha ambazo hazina sifa zimeondolewa kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) na uhakiki zaidi utafanywa kubaini kaya zilizoingizwa kwenye mpango huo zisizo na sifa ili ziondolewe.
Hayo yalisemwa jana wilayani Ngorongoro na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha ,Richard Kwitega kwenye kikao cha kutathimini utekelezaji wa Tasaf awamu ya tatu pamoja na Programu ya OPEC awamu ya tatu ambapo mipango yote hiyo inalenga kuzisaidia kaya masikini kujikwamua kiuchumi.
Kwitega ameagiza watendaji wote waliohusika kuingiza kaya zisizo na sifa kwenye mpango huo wachukuliwe hatua za kinidhamu ikiwemo kurejesha fedha hizo ili zitumike kusaidia sehemu nyingine.
Alisema kaya 44,643 ziliandikishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015 na zilistahili kupata malipo ya kwanza Julai na Agosti mwaka 2015 ambapo zilipokelewa Sh bilioni 1.8.
Alisema mpaka sasa mkoa umepokea awamu tisa za malipo ya ruzuku kwa kaya masikini ambapo Sh bilioni 17.1 zimeshapokelewa na kati ya hizo Sh bilioni 15.3 zimehaulishwa kama ruzuku kwa walengwa huku Sh bilioni 1.8 zimetumika kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli za mpango huo.
Pamoja na mafanikio ya Tasaf awamu ya tatu imeelezwa kuwa bado yapo maeneo ambayo wananchi wanahitaji kusaidiwa katika kujikwamua na umaskini uliokisiri. Naye Kaimu Mkurugenzi wa Tasaf, Omari Malilo, amezitaka halmashauri za wilaya kukamilisha miradi hiyo kabla ya Februari, 2017.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment