Image
Image

Migogoro ya ardhi Arusha pasua kichwa, kamati ya ulinzi na usalama yaanza kutafuta ufumbuzi.

KAMATI za ulinzi na usalama za mikoa ya Arusha na Kilimanjaro zimefanya ziara ya pamoja kukagua na kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa migogoro ya ardhi baina ya wilaya za Longido, Arumeru na Siha inayotishia uvunjifu wa amani.
Tayari baadhi ya athari za uwepo wa migogoro hiyo zimeainishwa ikihusisha wakulima na wafugaji, wananchi na mwekezaji kampuni ya Utalii ya Ndarakwai wilaya ya Siha na wananchi wa Longido na mwingine uliopo mahakamani.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Saidi Mecky Sadiki na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, wameziongoza timu za wataalam wa ardhi wa mikoa hiyo kukagua mipaka iliyotolewa na serikali mwaka 1954.
Katika kutafuta uhalali wa mipaka hiyo, timu za wataalamu zilisoma ramani zilizoainishwa na tangazo la serikali namba 135 la mwaka 1954 ambalo limeainisha mipaka hiyo kisheria na kuonesha baadhi ya vijiji kuwa wilaya gani.
Ziara hiyo ni utekelezaji wa agizo la waziri mkuu, Majaliwa Kasim Majaliwa aliyotaka serikali za mikoa hiyo kukutana na kujadiliana ili kumpa mapendekezo ya nini kinaweza kufanyika kumalizika kwa migogoro hiyo.
Wakuu wote wa mikoa walikiri kuwapo kwa timu kadhaa za wataalam za mwaka 2007 na 2012 ambazo zilitoa mapendekezo kadhaa ingawa baadhi yake bado hayajarejeshwa mikoa husika.
Akitoa majumuisho ya timu za wataalamu wa ardhi wa mikoa hiyo, Mpima wa mkoa wa Arusha, Hamdun Mansoor alisema hakuna mipaka mipya iliyowekwa tangu tangazo la serikali la mwaka 1954 na kukiri changamoto ya kutozingatiwa kwa tangazo la mwaka 1954.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment