Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka Hospitali ya Apolo, Bangalore ya Nchini India Sathyaki Nambala akiongea na waandishi wa habari leo kwa kuipongeza Serikali ya Tanzania jinsi ilivyowekeza katika matibabu ya moyo jambo lililosababisha wagonjwa wengi kutibiwa hapa nchini ukilinganisha na miaka ya nyuma. Kushoto ni Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa.
Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa akiongea na waandishi wa habari leo jinsi JKCI kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Hospitali ya Apolo, Bangalore ya Nchini India walivyofanya upasuaji wa kuvuna mishipa ya damu mguuni na kuipandikiza katika mishipa ya moyo iliyokuwa imeziba, kubadilisha milango ya moyo (Valves) ambayo haikuwa inapitisha damu vizuri. Kutoka kushoto ni Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka Hospitali ya Apolo, Bangalore Sathyaki Nambala.
Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka Hospitali ya Apolo, Bangalore ya Nchini India Sathyaki Nambala (katikati) akiwaonyesha mchoro wa moyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Prof. Mohamed Janabi na Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo Bashir Nyangasa wakati alitembelea ofisini kwa Mkurugenzi leo kwa ajili kumuaga baada ya kumaliza kambi ya upasuaji ya siku tano iliyofanyika katika Taasisi hiyo.
Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka Hospitali ya Apolo, Bangalore ya Nchini India Sathyaki Nambala (katikati) akiongea jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Prof. Mohamed Janabi na Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo Bashir Nyangasa wakati alitembelea ofisini kwa Mkurugenzi huyo leo kwa ajili kumuaga baada ya kumaliza kambi ya upasuaji ya siku tano iliyofanyika katika Taasisi hiyo.
Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa akiongea na waadishi wa habari jinsi JKCI kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Hospitali ya Apolo, Bangalore ya Nchini India walivyofanya upasuaji wa kuvuna mishipa ya damu mguuni na kuipandikiza katika mishipa ya moyo iliyokuwa imeziba, kubadilisha milango ya moyo (Valves) ambayo haikuwa inapitisha damu vizuri. Kutoka kushoto ni Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka Hospitali ya Apolo, Bangalore Sathyaki Nambala na kulia ni Dkt. Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Peter Kisenge.
Picha na Anna Nkinda - JKCI
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment