Waziri wa Habari, utamaduni, Sanaa na Michezo
Mh.Nape Nnauye amezindua Program ya mfuko wa kusaidia timu za Taifa wenye
jukumu la kubuni vyanzo mbalimbali vya rasilimali na kuwataka watanzania kwa
umoja wao, Sekta binafsi na familia ya wanamichezo kuunga mkono juhudi hizo.
Akizungumza na wanahabari 23 February 2017 jijini Dar es Salaam Waziri Nape amesema kuwa wao kama serikali na kama sehemu ya wadau hawatasita
kusimama hadharani na kunyoosha kidole kama mambo hayataenda sawa, kutokana na
wanataka wajenge mfumo ambao wadau watafikia mahali wawaamini kwamba mambo hayo
yanasimamiwa na yanaenda vizuri.
Amesema imani ya serikali katika ubunifu huo ni
matumaini yao kwamba jambo hilo litakwenda vizuri na kupatikana matokeo wanao
yakusudia.
"Msisite
kuchukua hatua mapema pale ambapo kutaonekana hata mashaka kido juu ya utendaji
ni vizuri tukachukua hatua mapema ili tusije tukaonekana na sisi ni sehemu ya
tatizo, jambo hili zuri likisimamiwa vizuri litatupa matokeo mazuri, jambo hili
zuri likisimamiwa vibaya linawezekana likawa ni kaburi la kuzika juhudi
mbalimbali zitakazo jitokeza za kujaribu kutafuta fedha yakufainest michezo
katika nchi yetu"Nape.
Waziri Nape AmempongezaMkuu wa kitengo cha Maendeleo ya Soka cha Shirikisho la soka Tanzania (TFF).Serengeti Boys Kim Poulsen kwa kazi nzuri anayo fanya pamoja na wenzake, huku
akisema kuwa Serengeti Boys wao kama serikali wana matumaini makubwa na timu
hiyo kwa kuwa timu ni nzuri na hakuna sababu ya kushindwa.
"Watanzania kwa pamoja tukishikamana tunayotimu
nzuri hatunasababu ya kushindwa, watanzania tupunguze tabia ya kunyoosha vidole
vibaya, kama kuna mabaya bakinayo moyoni mwako tuseme mema juu ya Serengeti
Boys na naamini tutafanikiwa"Nape.
Pia amesema suala hilo serikali haitasita kuingiza
mkono kuhakikisha kwa namna yeyote iwe kwa hamasa kwa rasilimali kuwa Serengeti
Boys inaenda kupiga kambi na ifanye vizuri kwenye maandalizi yake kwenda Gabon
na wanaimani itafanya vizuri.
Ameongeza kwa kusema kuwa alikuwa anaongea na rais
wa TFF hivi karibu kwamba serikali itaangalia uwezekano wa kuwa na kamati ya
hamasa kwa ajili ya kuhakikisha inasapoti Serengeti Boys na kuhakikisha
inafanya vizuri Gabon.
Safari hii haendi mwalimu Posen na watu wake,
haiendi Serengeti Boys peke yake, watanzania tunakwenda Gabon,watanzania kwa
pamoja, kwa dua zetu kwa rasilimali zetu na kila kitu tunachoweza na hata
kamati za ufundi zikiweza lakini kikubwa kuliko yote safari hii watanzani
tunataka kwenda gaboni wenyewe tuhakikishe tunarudi na ushindi"Nape.
0 comments:
Post a Comment