Na Anna Nkinda - JKCI
14/3/2017 Jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ushirikiana na madaktari wenzao wa Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Upasuaji wa Moyo ambaye pia ni Daktari bingwa wa upasuaji wa Moyo Bashir Nyangasa wakati akielezea jinsi kambi hiyo ya upasuaji inavyoendelea kutoa matibabu kwa wagonjwa.
Dkt. Nyangasa alisema, “Kwa kushirikiana na washirika wetu wa OHI tulianza kambi maalum ya upasuaji kuanzia tarehe 10/03/2017 hadi leo tarehe 17/3/2017 tumefanya upasuaji kwa wagonjwa 11 ambao wanaendelea vizuri, kati ya hao watoto ni tisa na watu wazima ni wawili”,.
Dkt. Nyangasa alisema katika kambi hiyo ambayo inamalizika tarehe 17/3/2017 walipanga kufanya upasuaji kwa wagonjwa 25 kati ya hao watoto ni 15 na watu wazima ni 10.
Kuhusu uhitaji wa damu kwa wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji wa Moyo Dkt. Nyangasa alisema wagonjwa hao wanahitaji damu nyingi hivyo basi aliwaomba wananchi wajitokeze kuchangia damu ambayo itatumika kwa wagonjwa.
“Tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kuchangia damu na uchangiaji huu wa damu usifanyike mara moja bali uwe endelevu kwani Taasisi inatoa huduma kwa wagonjwa wakati wote siyo wakati wa kambi maalum za matibabu ya moyo pekee yake”, alisisitiza Dkt. Nyangasa.
Tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2017 JKCI kwa kushirikiana na baadhi ya washirika wake wa nje ya nchi ambao ni Madaktari Afrika wa Marekani, Hospitali za Apolo Bangalore na BLK zote za nchini India na Open Heart International ya Australia wamefanya matibabu ya moyo ya kufungua na bila kufungua kifua kwa wagonjwa wa moyo wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.
Home
Afya
Slider
Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete na taasisi ya open heart ya nchini Australia yafanya upasuaji.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment