Dar es Salaam
Kufuatia kusambaa kwa taarifa kupitia mitandaoni hivi leo zikidai kuwa Mwanachama na Kada mkongwe wa CCM Chrisant Mzindakaya amefariki dunia hatimaye taarifa hizo zimekanushwa na mwanasiasa huyo.
Mapema hivi leo Mwanasiasa huyo amezungumza na vyombo vya habari katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete nakusema kuwa yeye yupo imara kiafya hivyo wasambazaji wa taarifa hawana nia njema.
Mzindakaya ameongeza kwa kusema amesikitishwa mnoo na taarifa hizo ambazo zimezua taharuki na kuwaita wasambazaji wa taarifa hizo kuwa ni wapumbavu nakwamba muda wowote kuanzia sasa ataruhusiwa kuondoka hospitalini hapo.
"Madaktari wamenileza Afya yangu imeimarika mfano wa kijana wa miaka 20, hivyo ntaruhusiwa kutoka hospitalini hapa mda wowote.Amesema Mzindakaya.
Mwenyezimungu ampe umri mrefu zaidi Mwanasiasa huyu.
0 comments:
Post a Comment