Kauli hiyo ya Rais imeelezwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu mkoani Dodoma nakusema Rais Dkt.John Pombe Magufuli ameamua madaktari hao waajiriwe nchi baada yakupatikana kwa fedha za kuwawezesha kuajiriwa.
Vilevile Waziri aliongeza kwa kusema kuwa uamuzi huo wa Rais wa kutaka Madaktari hao waajiriwe nchini badala ya nchini Kenya kama ilivyokuwa awali nikutokana pia na kukutwa na sifa stahiki za kupatiwa ajira nchini.
Madaktari hao 258 ambao wanapatiwa ajira nchini Tanzania ni kati ya Madaktari 496 waliokuwa wameomba kuajiriwa nchini Kenya, kufuatia Serikali ya Kenya kuingia kwenye mzozo na Madaktari wa nchi hiyo na kuamua kutangaza ajira katika nchi jirani.
0 comments:
Post a Comment