Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutambua usawa wa haki kwa watu wenye tatizo la mtindio wa ubongo, na kuwapatia fursa sawa kutoa mchango katika jamii.
Bw. Guterres ametoa wito huo jana kwenye maadhimisho ya siku ya mtindio wa ubongo, akisema uwezo wa kisheria na utambuzi kwa usawa mbele ya sheria, ni haki ya kimsingi ya watu wenye tatizo la mtindio wa ubongo kama watu wengine kwenye jamii.
Bw. Guterres ametaka uungaji mkono wa lazima kwa watu wenye tatizo hilo, ili waweze kufanya maamuzi yao wakati wakitenda haki na uhuru wao.
Umoja wa mataifa umeitaja Aprili 2 kila mwaka kuwa siku ya mtindio wa ubongo duniani, ili kutoa mwamko wa kuboresha maisha ya watu wenye tatizo hilo.
Home
Kimataifa
Slider
Guterres atoa wito kwa UN kutambua usawa wa haki kwa watu wenye tatizo la mtindio wa ubongo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment