Image
Image

Magufuli:Wenye vyeti feki 9932 waondolewe kazini,ajira zitangazwe wenye sifa waziombe.

Watumishi wa Umma waliobainika 9932 waliobainika kugushi vyeti wameamuriwa kuondolewa kazini kuanzia leo na mishahara yao ya mwezi huu kukatwa. 
Kauli hiyo ameitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli baada ya kukabidhiwa Ripoti ya watumishi wa Umma wasio na sifa Katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma hivi leo.
"Mshahara wao wa mwezi huu ukatwe na waondoke mara moja kwenye utumishi wa umma kuanzia leo, watakao baki mpaka tukaingia mwezi wa tano muwapeleke kwa mujibu wa sheria ili kusudi wakafungwe hiyo miaka saba, hatuwezi kuwa na taifa la wafanyakazi wasio na sifa.Rais Magufuli.
Dkt Magufuli Pia amesema kuwa nafasi hizo 9932 ambazo zilikuwa hewa sasa baada ya kuondolewa kwa watumishi hao zitangazwe kusudi wenye sifa waombe.
Dkt.Magufuli amewataka wanahabari kuchapisha majina yao kwenye magazeti kusudi waweze kujulikana na kusisitiza kuwa anataka watu wajifunze.
"Wametuibia hela kwa kipindi chote walichofanya kazi hawana sifa lakini wamekaa kwenye nafasi ambazo hawastahili kuwa hapo, haya ni majambazi ni majizi kama yalivyo majizi mengine.RaisMagufuli.
Rais Dkt.Magufuli ameongeza kwa kusema kuwa Jumla ya watumishi wa umma 1538 mishahara yao ya mwezi huu imezuiliwa baada ya kuibuka kwa utata wa vyeti vyao kutumiwa na zaidi ya mtu ya mmoja.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment