Mchezaji huyo anayeng’ara kwa sasa alijiunga na Kagera akitokea Simba ingawa katika siku za hivi karibuni amekuwa akikanusha kwamba hayupo kwa mkopo kama Wekundu hao wanavyodai bali yuko kimkataba.
Straika huyo anasema kwamba huu si muda wake wa kwenda Simba kuuza sura bali anataka sehemu ambayo atacheza na kushindana kama anavyofanya sasa hivi akiwa chini ya usimamizi wa Mecky Maxime ambaye ni kocha kijana wa Kagera na George Kavila kama nahodha.
Ikumbukwe kwamba baada ya ligi kumalizika msimu uliopita kulitokea mgogoro kati ya Mbaraka na uongozi wa Simba ambao walidai kuwa mchezaji huyo ana mkataba nao na kumshitaki katika Shirikisho la Soka nchini (TFF) ambao waliwaambia pande zote tatu ambazo ni mchezaji, Simba na Kagera waliokuwa wamempa mkataba wakae chini ili kumalizana.
Akizungumza na Mwanaspoti, Mbaraka ambaye amefikisha mabao 12 sawa na winga wa Yanga, Simon Msuva alisema kuwa mpaka sasa hajafikiri kurejea Simba na anaamini kuwa akienda hatapata nafasi ya kucheza kwani latika nafasi yaketayari kuna nyota kama Laudit Mavugo na Ibrahim Ajib.
“Mimi ni mchezaji wa Kagera Sugar na nilisaini nao mkataba wa mwaka mmoja sio kwamba nilikuja huku kwa mkopo, mkataba wa mkopo ulimalizika muda mrefu. Simba ina wachezaji wazuri wanaocheza mimi nitakwenda kucheza wapi.
“Kuwasilikiza wakija nitawasikiliza lakini kitendo cha kurudi kucheza hapo ndiyo tatizo mimi nataka nicheze kama ilivyo huku pale haitakuwa rahisi, sitaki kukaa jukwaani, nimewaachia wale wanaopenda kucheza Simba ama wanaotaka wasikike kuwa wapo Simba wakati hata nafasi hawapati,” alisema Mbaraka kwa kujiamini ingawa Simba wana uhakika kwamba lazima avae jezi Msimbazi msimu ujao.
Mbaraka alisema kuwa kwasasa anafikiri kucheza timu ambazo zitampa nafasi ya kucheza maana anataka kuweka rekodi ya ufungaji kama ilivyo kwa wachezaji wengine ambao wamewahi kutwaa Kiatu cha Dhahabu.
“Nina mawazo ya kuwa Mfungaji Bora kwasasa, sihofii akina nani nakimbizana nao, namuomba Mungu anisimamie nifanikamilishe ndoto zangu, bado nayakumbuka yaliyonikuta Simba,” alisema Mbaraka ambaye ni miongoni mwa wachezaji wenye kipaji lakini ana umbo dogo. Simba imemuweka mchezaji huyo katika malengo yake ambapo kamati ya usajili imejiridhisha kwamba ameiva tayari kwa mashindano makubwa na akitua kwenye kikosi cha sasa cha Simba atapata namba. Wekundu hao wamejidhatiti kupata nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa mwakani ambapo wakishakamilisha azma hiyo ndipo watakapoanza usajili wao mpya kujiweka sawa ambapo sasa walichofanya ni kupiga kambi kwenye mechi mbili zilizosalia Kanda ya Ziwa dhidi ya Mbao na Toto Afrika kujiweka pazuri.
0 comments:
Post a Comment