Ujumbe wa Kampuni hiyo ambayo imewekeza katika kilimo cha kisasa katika Mataifa mbalimbali Dunia ikiwemo Amerika, Afrika, Ulaya na Asia wamekutana na Kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam na kumweleza dhamira ya kutaka kuja kuwekeza nchini.
Ujumbe wa Wawekezaji hao kutoka Indonesia ambao umeongozwa na Mchugaji Dakta VERNON FERNANDES wa World Agape Ministries umemweleza Makamu wa Rais kuwa wanania ya dhati ya kuwekeza Tanzania na wanataka kupata ardhi kubwa kwa ajili ya kilimo cha kisasa ambacho kitakwenda pamoja na usindikaji wa mazao hao ili kuondoa tatizo la kusafisha malighafi nje ya nchini.
Amesema mpaka sasa wameshatembelea maeneo mbalimbali nchini ikiwemo mkoa wa Morogoro lakini wanakutana na changamoto kubwa ya kukosekana kwa eneo la kutosha kwa ajili ya uwekezaji huo.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameonyesha kufurashishwa na nia ya wawekezaji hao kuja kuwekeza kwenye sekta ya kilimo cha kisasa nchini.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema uwekezaji huo mkubwa ukianza nchini utatoa fursa ya ajira kwa watanzani wengi na kuongeza pato la taifa na wawekezaji wenyewe.
Makamu wa Rais pia amewaahidi wawekezaji hao kuwa atashughulikia haraka kupatika kwa eneo la ardhi kwa ajili ya uwekezaji huo ili kazi ya kujenga miundombinu kwenye eneo la uwekezaji ianze mara Moja.
Ameeleza kuwa Tanzania ina eneo kubwa na zuri kwa ajili ya kilimo hasa kilimo cha umwagiliaji ambalo bado halijaendelezwa hivyo kama wawekezaji wengi watajitokeza kuwekeza kwenye eneo hilo taifa litajitosheleza kwa chakula na kuuza ziada nje ya nchini.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais.
Ikulu – Dar es Salaam.
6-April-2017.
0 comments:
Post a Comment