Msani wa Hip hop nchini Tanzania Roma Mkatoliki inaelezwa amekamatwa usiku wa kuamkia hivi leo akiwa studioni kwake Tongwe Recods, na kuchukuliwa na watu wasiojulikana.
Kupitia taarifa ya mbunge wa Mikumi Joseph Haule na ambaye pia ni msanii maarufu kama Prof. Jay, kupitia kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram aliandika taarifa za kukamatwa msani huyo nakusema Roma Mkatoliki, Moni Centrozone na kijana mmoja wa kazi walikamatwa wakiwa studio za Tongwe Records.
"Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za Tongwe Records majira ya saa moja usiku na wamemchukua Roma, Moni na kijana wa kazi na pia wamechukua Computer ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana, Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi" aliandika Prof. Jay.
Kupitia kwenywe mitandao ya kijamii nchini Tanzania habari inayozungumzwa ni hiyo ya kukamatwa kusiko julikana kwa msanii huyo na wenziwe, huku wengine wakichagiza na siasa, kutokana na msanii huyo mara kadha kuwa akitoa nyimbo zake zenye kuonesha kuisema serikali ama jambo ambalo linazungumziwa.
Mara kadhaa wafuasi wa msanii huyo haswa mashabiki wamekuwa wakimuita shuja asiyeogopa kusema kupitia tungo zake za mashairi ya mziki,huku wengine wakienda mbali na kusema labda huenda amekamatwa kufuatia moja ya wimbo wake unaoendelea kusambaa mitandaoni unaoitwa USINIPANGIE ambao unamashiri kuntu ndani yake kama wasemavyo vijana.
Naye Kiongozi Mkuu wa ACT na Mbunge wa Kigoma mjini Mh.Zitto Kabwe ameguswa na kukamatwa kwa msanii Roma Mkatoliki, kupitia ukurasa wake wa Twitter akayaandika haya.
”Uvamizi wa studio ya Tongwe na kumkamata msanii Roma Mkatoliki ni mwendelezo wa uongozi wa kigangstar na lazima kulaani Kwa nguvu zetu zote.” – Zitto Kabwe.
Msanii Nay wa Mitego baada ya kupata taarifa za kukamatwa kwa Roma Mkatoliki kayaandika haya.
”Kuvamia Ofisi Za watu, heh.! Kumbe nayo ni Kazi.?! Nina Imani uko salama mwanangu, Kamanda @roma2030 Sina ata chembe ya wasi wasi. #Wapo.” – Nay wa Mitego.
Hivi karibuni msanii wa Hip hop Emannuel Elibariki a.k. Nay wa Mitego, alikamatwa na polisi akiwa mkoani katika shughuli zake za muziki, akituhumiwa kuimba wimbo wenye kukashifu Serikali, lakini siku moja baadae Rais wa Tanzania kupitia kwa waziri wa Michezo Harrison Mwakyembe aliamuru kuachiwa kwa msanii huyo kwani alichokiimba hakina tatizo ni kazi ya sanaa, huku akidai rais anaupenda wimbo huo na kumtaka aongeze mashairi kdhaa ikiwamo wakwepa kodi nk.
Msanii Nay wa Mitego, amekuwa mwenye kuimba nyimbo zenye kugusa hisia za wengi na hivyo kutafsiriwa kwa namna tofauti, lakini wimbo wake wa wapo umekuwa maarufu kwa kusikilizwa mnoo ndani na nje ya Tanzania.
Nay wa Mitego siku chache hizi kupitia ukurasa wake wa Instagram alipachika ujumbe wa maneno ukidai kuwa wapo watu wanamtisha.
Home
BURUDANI
Slider
Kukamatwa kwa Roma, Prof. Jay, Zitto Kabwe na Msanii Nay wa Mitego wazungumza haya.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment