Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo 10 Aprili, 2017 Ameteua wajumbe wa kamati maalum ya pili itakayo fanya uchunguzi wa madini yaliyomo kwenye mchanga wenye madini ulio ndani ya makontena yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Katika taarifa ya IKULU kwa vyombo vya Habari, Kamati hiyo inajumuisha wachumi na wanasheria na imetanguliwa na kamatiya kwanza iliyoundwa na wataalamu wa masuala ya jiolojia, kemikali na uchambuzi wa kisayansi.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imewataja wajumbe wa kamati hiyo kuwani;
1. Prof. Nehemiah EliachimOsoro
2. Prof. Longinus KyaruziRutasitara
3. Dkt. Oswald Joseph Mashindano
4. Bw. Gabriel Pascal Malata
5. Bw. Casmir Sumba Kyuki
6. Bi. ButamoKasuka Philip
7. Bw. UsajeBenardUsubisye
8. Bw. Andrew Wilson Massawe
Wajumbe hao wataapishwa na Mhe. Rais Magufuli kesho tarehe 11 Aprili, 2017 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
10 Aprili, 2017
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment