Image
Image

Serikali haitawavumilia wenye vyeti feki, yatangaza ajira 4300 za elimu nchini.

Zaidi ya watumishi 4,300 wapya wanataajiriwa kuajiriwa katika kada ya elimu na wasanifu wa maabara ambapo ajira hizo mpya zinakuja bada ya kukamilika kwa zoezi zima la uhakiki watumishi hewa lililokuwa likiendelea.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma Mh. Angela Kairuki ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi na wanachuo mkoani Tabora ambapo amesema kwa muda mwingi taifa limekuwa likikabiliwa na changamoto ya watumishi hewa huku likipoteza fedha nyingi.
Aidha Mhe. Kairuki amesema kuwa kamwe serikali haitamvumilia mtumishi ambaye atabainika kuwa na vyeti feki, huku akiwataka watanzania kutambua madhara ya vyeti hivyo kuwa ni kutopatikana kwa huduma stahiki huku akiwataka wahitimu katika kada mbali mbali kutowaonea haya watu ambao wanataka kupora ajira za wenzao.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment