Image
Image

Timu ya Yanga yaiadhibu Azam bao 1-0 katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC wameibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo uliochezwa leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuifanya klabu hiyo kuwa kileleni mwa ligi.
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC wameibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo uliochezwa leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuifanya klabu hiyo kuwa kileleni mwa ligi.
Katika kipindi cha kwanza cha mchezo Azam FC waliweza kumiliki mpira kwa asilimia 54 huku Yanga wakimiliki mchezo kwa asilimia 46, dakika ya 14 ya mchezo Vicente Bossou alipewa kadi ya njano, dakika 28 ya mchezo Zulu alitolewa nje baada ya kuumizwa na kuingi Emanuel Martin kuchukua nafasi yake . 
Baada ya hapo mabadiliko hayo yalifanya Niyonzima kurudi namba nane , Emanuel alikwenda juu kama mshambuliaji namba mbili kwa Obrey Chirwa, kufuatia mabadiliko haya ndiyo kidogo yalianza kuleta nguvu na kuwafanya Yanga kuanza kucheza soka kwa kuonana. 
Mpaka wanakwenda mapumziko Yanga haikubahatika kupata goli wala Azam FC haikubahatika kuona lango la Yanga. 
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu zote mbili huku Yanga wakiwa na nguvu na uwezo zaidi jambo lililopelekea Yanga kumiliki mpira kwa asilimia kubwa katika kipindi cha pili.
Katika dakika ya 52 ' Nadir Canavro alipata kadi ya njano. Na kupelekea walinzi wote wa kati wa Yanga kuwa na kadi za njano . Wakati huo huo Deusi Kaseke alitoka nje na kuingia Geofrey Mwashuiya.
Yanga iliendelea kuwasumbua Azam FC na katika dakika ya 70 mchezaji Obrey Chirwa aliipatia Yanga goli la kuongoza ambalo lilidumu kwa dakika zote tisini na kuifanya Yanga kuibuka na point tatu muhimu katika mchezo huo na kuifanya Yanga kuwa na pointi 56 na kukaa kileleni mwa ligi, huku Simba ikishika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi. 
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment