Image
Image

BreakingNews:Rais Magufuli ateua mkurugenzi mtendaji TIC na katibu tawala mkoa wa Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli amemteua Bw.Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Kabla ya Uteuzihuo Bw. Geoffrey Idelphonce Mwambe alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni itajazwa baadaye.
Wakati huo huo, Mhe.Rais Magufuli amemteua Bw.Clifford Tandari kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro.
Bw.Clifford Tandari anachukua nafasi ya Dkt.John Ndunguru ambaye amestaafu.
Kablayauteuzi huo Bw.Clifford Tandari alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Uteuzi wa viongozi hao unaanza maramoja.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,IKULU
Dar es Salaam
17 Mei, 2017

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment