Image
Image

Mwigulu:Majeruhi,Mahututi na mwenye majeraha watibiwe kwanza bila PF3.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema kwamba kuanzia sasa kama serikali wameamua kuwa Majeruhi, Mahututi asiyeweza kutoroka,na mtu mwenye majeraha yasiyo na utata wapewe matibabu KWANZA bila PF3.
Waziri Nchemba ameyasema hayo kupitia andiko lake alilolipachika kupitia ukurasa wake wa Facebook huku akisisitiza hatua za kufuata, nakusema PF3 inaanza mara moja wakati mgonjwa akiendelea kupewa matibabu ambapo anasema uamuzi huo kama serikali unalenga kuokoa maisha yao kwanza.
Aidha waziri Mwigulu ameongeza kwa kusema kuwa, Utaratibu huu unajicho la karibu kutoka kwenye vyombo vya usalama ili kubaini ukweli jeraha la mhusika.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment