Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Boniventure Mushongi amethibitisha kutokea kwa mauaji ya mtu mmoja ambaye amepigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Kibiti mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo zinasema mtu huyo aliyeuawa ni kiongozi wa Chama Cha Mapinduzi ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CCM tawi la Njia nne wilayani Kibiti.
Kamanda wa Polisi Pwani wakati anaongea kwenye kipindi cha East Africa Breakfast cha East Africa Radio amethibitisha kutokea mauaji hayo ingawa yeye hajataka kuweka wazi aliyeuwawa ni nani na kusema wakifika eneo la tukio ndipo watajua ni nani aliyefariki na kutoka taarifa rasmi.
Sikiliza hapa.
0 comments:
Post a Comment