Rais Dkt. John Magufuli amefanya ziara katika ofisi za shirika la Utangazaji Tanzania – TBC 16 May 2017 ambapo ametembelea maeneo kadhaa kujionea hali ilivyo pamoja na kuzungumza na wafanyakazi.
Akizungumza na wafanyakazi wa TBC Dkt. Magufuli amewataka wafanyakazi hao kuwa na umoja na mshikamano na kujituma ili kuboresha huduma wanayoitoa.
Rais pia amezungumzia mkataba wa TBC na Star Times ambapo amesema mkataba huo utapitiwa upya na ukibainika kuwa na mupungufu utasitishwa mara moja.
Katika ziara hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt.Ayub Rioba amemweleza Rais Dkt. Magufuli kwamba TBC inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo uhaba wa vitendea kazi, uchakavu wa miondombinu jambo ambalo Rais Dkt. Magufuli ameahidi kuchukua hatua za kutatua changamoto hizo.
Dokta Magufuli amefanya ziara kwa mara ya kwanza katika shirika la utangazaji nchini tangu aingie madarakani.
0 comments:
Post a Comment