Baadhi ya Wabunge wameomba kuundwa kwa Kamati maalumu itakayopitia upya vitabu vyote vilivyosambazwa katika shule mbalimbali nchini kuanzia darasa la Kwanza hadi kidato cha sita kufuatia kuwepo kwa makosa mengi kwenye vitabu hivyo.
Wabunge hao wametoa ombi hilo wakati wakichangia bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa Fedha wa 2017/2018, ambapo mjadala mkali umejitokeza kuhusu uwepo wa vitabu vyenye makosa pamoja na wanafunzi wa kike wanaopata ujauzito wakiwa shuleni.
Katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2017/2018, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inahitaji zaidi ya Shilingi Trilioni Moja Nukta Tatu kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake mbalimbali.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment