Image
Image

Serikali kumwaga ajira 15,000 kwa watumishi.

SERIKALI itamwaga ajira 15,000 kwa watumishi wa kada mbalimbali serikalini kabla ya Juni 30, mwaka huu.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Laurean Ndumbaro akizungumza na vyombo vya habari kwenye Ukumbi wa Habari wa Bunge, alisema ajira hizo ni za mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, mwaka huu na uchambuzi unaoonesha kila kada itapata watumishi wangapi utatolewa baadaye.
Ajira hizo zinatolewa kama sehemu ya ajira zaidi ya 71,496 ambazo serikali iliahidi katika bajeti ya mwaka 2016/17 na imekuwa ikizitoa kila wakati kwa kada tofauti kadiri ya mahitaji. Ndumbaro alisema ajira hizo zitakapotangazwa, kabla ya mtumishi kuajiriwa atatakiwa kuwa na vyeti vyote halali vya kidato cha nne na sita na cha taaluma waliyosomea kinachoonesha elimu yake. “Watumishi watakaojitokeza kutaka kuajiriwa katika kada mbalimbali serikalini, watatakiwa kuwa na vyeti hivyo na lazima viwe vimehakikiwa ama na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) au vyuo alichosoma muombaji iwe chuo kikuu, taasisi au chuo cha ufundi,” alieleza Dk Ndumbaro.
Hadi sasa Serikali imeajiri walimu wa sayansi na hesabu wa sekondari 3,081 na madaktari 258, na kwa kutolewa ajira hizo 15,000, kutaongeza idadi ya ajira kwa watumishi kabla ya kumalizika mwaka huu wa fedha. Katika Siku ya Mei Mosi iliyofanyika kitaifa mkoani Kilimanjaro, Jumatatu wiki hii, Rais John Magufuli aliahidi kwamba Serikali itarudisha utaratibu wa kutoa nyongeza za mishahara kila mwaka na kupandisha madaraja watendaji wake. Alisisitiza kuwa, baada ya kuondolewa wafanyakazi hewa na wale wenye vyeti feki, Serikali sasa imejipanga kuhakikisha inatoa ajira mpya kwa watu 52,000. “Tutaajiri walimu, wauguzi na wafanyakazi wa kada nyingine,” alisema.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment