WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, amemwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Inspekta Jenerali Ernest Mangu, achunguze tukio la askari polisi anayedaiwa kufyatua hovyo risasi na kumtisha kwa risasi, aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima.
Mwigulu aliyasema hayo katika viwanja vya Bunge alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kumtaka atoe kauli kuhusu tukio hilo.
Nchemba amesema kwa sasa hawezi kutoa tamko lolote hadi pale atakapopata taarifa kamili kwa pande zote kuhusu nini hasa kilichotokea hadi kuibuka kwa hali hiyo ya kufyatuliana risasi.
Home
News
Slider
Waziri Nchemba amuagiza IGP Mangu kuchunguza tukio la polisi anayedaiwa kufyatua risasi kwa Malima.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment