Image
Image

Rais Magufuli apokea hati za utambulisho za Mabalozi wa nchi tatu.





Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Oktoba, 2017 amepokea hati za utambulisho za Mabalozi watatu waliopangiwa kuziwakilisha nchi za Oman, Uholanzi na China hapa nchini.
Waliowasilisha hati zao kwa Mhe. Rais Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam ni Mhe. Ali Abdullah AlMahruqi – Baloziwa Oman hapanchini, Mhe. JeroenVerheul – Balozi wa Uholanzi hapa nchini na Mhe. Wang Ke – Baloziwa China hapa nchini.
Mhe.RaisMagufuli amewapongeza Mabalozi hao kwa kuteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapanchini na amewahakikishia kuwa Serikali yake itafanya kazi nao kwa ukaribu ili kuendeleza na kukuza zaidi ushirikiano kati ya nchi hizo na Tanzania hususani katika uchumi.
“Nimefurahishwa sana na ziara iliyofanywa na Mawaziri wa Oman hapa nchini,naomba ufikishe shukrani zangu kwa Mfalme wa Oman Mtukufu Sayyid Qaboos bin Said Al Said, naamini yote tuliyo zungumza ikiwemo kubadilishana uzoefu katika mafuta na gesi, uwekezaji katika viwanda na ujenzi wa miundombinu tutayatekeleza kwa manufaa ya wananchi wa nchi zetu” amesemaMhe.
Rais Magufuli alipozungumza na Balozi Ali Abdullah Al Mahruqiwa Oman.
Mhe. Rais Magufuli amemuambia Balozi Jeroen Verheulwa Uholanzi kuwa Tanzania inayogesi nyingi na itafurahi kupokea wawekezaji kutoka Uholanzi ikizingatiwa kuwanchihiyo inauzoefu na teknolojia kubwa katika sektahiyo.
Kwa upande wa Baloziwa China hapa nchini Mhe. Wang Ke, Mhe. Rais Magufuli amesema uhusiano wa Tanzania na China niwakihistoriana kidugu, hivyoametoa wito kwa Balozi huyo kuuendeleza na kuhakikisha fursa zenye manufaa kwa nchi zote zinatumiwa ipasavyo ikiwemo kukuza uwekezaji, biashara, utalii na ushirikiano katika usafiri wa anga.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment